Thursday, May 31, 2007

SEND OFF PARTY YA BI FLORA-AIRPORT NIGHT PARK


Aiingia kwa tabasamu la haja bi arusi mtarajiwa! akitembea kama anagombea nafasi ya kuiwakilisha nchi katika Miss World Beuty Contest!! huku akisindikizwa na mpambe wake wakiwa wamependeza na rangi nzuri ya pitch!! ingawa walichelewa kidogo kuingia ukumbini,kufuatia shughuli za kimila kuxhelewa kufikia ukingoni jioni ile,McNdimbo kama kawaida yake akaipeleka shughuli kwa ku-keep time! wakaanza kwa kufungua champaign af wakala keki na baadae utambulisho na nasaha fupi zilizoofuatiwa na burudani za kutosha kutoka upareni.. ''....ambiere ee.....mgothi eee.....'' wakaruka na sebene za kiroho na baadae wakaenda kula na kupata burudani ya show za wateule wa Mungu na mtaalam wa kuiga sauti za watu Bw Nyerere! Ama kwel "... burudani ni jadi yetu..."