Friday, December 14, 2007


Maisha kweli ni kama maua!
Tukiwa na furaha zetu hapo ndani ya UDSM uku tukiwaza jinsi ya kutoka na uhondo wa Rugemarila(now The Prof)......
Hakuna aliyekuwa akiamini kuwa siku moja mwenzetu Bi Neema,angetuacha!
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI..
Hata hivyo,gurudumu linaendelea;watano kati ya kundi hilo ni wanafunzi wa shahada ya uzamili katika fani mbalimbali...
Tusongeshe wanangu...kulima wengine hatuwezi!

Sunday, November 18, 2007

HARUSI YA BW. RICHARD MASUKE NA BI DINNA-Peace Of Mind TPDC Mikocheni tar 17 Nov,2007

"..kubyaala mawe,kubyaala cha widza..."
ilikuwa ni uhondo kutoka kwa DJ TEN akiwakamata wasukuma kwa kina walipokuwa wakiwa na furaha ya kupata binti mrembo mwenye asili ya kijita,aliyezamia mitaa ya Bariadi siku tele na kuwa na ladha ya kisukuma pia-Dinna..mweupe na ambaye kwa mila za kisukuma basi hiyo mahali yake ukiwa namfuko mwepesi hugusi. Ila kijana Richard akajipindua na kumtia kibindoni kwa furaha za ziada.
"...ndolelaaaaa...ndolela babaaaa...!" wasukuma wa kijita hao wakazunguka nao wakijifariji baada ya binti yao kuungana na familia ya kina Masuke.Wakicheza kwa furaha na kuongozwa na Ephraim Mafuru(Marketing manager wa Vodacom Tanzania),paliwa hapatoshi!!
Mtaalamu wa burudani McNdimbo,kama kawaida akiwapa wakati mgumu weasukuma wala kuketi katika viti vyao kila baada ya muda! kwa kweli ilikuwa burudani kwelikweli.
Shughuli hiyo ilisheheni wadau wa kutosha akiwamo Waziri wa mifugo,Mh.Diallo

SEND OFF PARTY YA BI.ABELA KAJUMULO LANDMARK HOTEL TAR 8,NOV,2007

Ilikuwa ni nderemo na furaha kwa wahaya wale na kuwa na uhakika na kupata mume tena wa kinyumbani! ilikuwa ni '...dereva babili...dereva babiliii eee...!' kili baada ya muda. wazazi wakiwa na furaha kweli na hasa Mama wa bibi arusi mtarajiwa a.k.a mama Tina,ambaye pia ni mama yake na mwigizaji maarufu wa filamu hapa nchini-Kanumba(ambaye alikuapo pia).
Shughuli ilianza na taratibu za mila na desturi za kihaya,wakwe wakaingia na mizigo ya kutosha;kabiya(beer),kasoda,bila kusahau kabhitoki(ndizi) na kakinywaji ka nyumbani. Ilikuwa ni burudani sana kuona wahaya hao,pamoja na usomi wao uliobobea,wakizama katika mila na desturi zao.
Baada ya majadiliano marefu ya hapa na pale kati ya mshenga na wazazi wa binti mtarajiwa waliruhusiwa kumleta bwana mtarajiwa ndani na kisha bi mtarajiwa akaingia kwa mbwembwe na shughuli ikaenda murua chini ya mikono salama ya mtaalam wa kuburrudissha hapa Africa ya mashariki na kati-McNdimbo 'mwana wa mshikemshike'
Pamoja nae alikuwapo Dr. Zero 'mzee wa dozi nene' kwa maharusi na show yake kali yenye vionjo vyote vya burudani;bongo flava,gospel,zilipendwa hadi segere! kudadadeki!!
ilikuwa ni uhondo toshaaa!

Tuesday, June 5, 2007

Juni 16 Ndo hiyoooooo!!


Ushawahi kuona mganga akajiganga!

Mbado!

Ushawahi kuona kinyozi anajinyoa tena ndani ya daladala!

Basi hayo ndo mambo ya Jun 16 pale ambapo McNdimbo almaarufu Mwana wa Mshikemshike atakapokua mbele ya altare pale CCT Chamlaincy-UDSM akiatamka kwa lugha ya kikwao

''...Yes I do...'' Huku kimwana wake alobarikiwa na Mwenyeeezi Mungu,mtoto mwenye mvuto na tabasamu la asili akinyoosha kidole chake cha mkono wa kushoto na kuvikwa ile golden wedding ring!

Wajua kitachofuata? ni vigelegele na makofi na vifijo na nderemo na ......

kutoka Mbeya na Arusha na Singida na Dodoma na Songea na Bukoba na Mwanza na hapahapa jijini af vya ziada kutoka kule USA

Ni burudani ya kutosha sasa itakayofuatia pale Sinza Kijiweni kwa Vatcan City Hall na hao waburudishaji wa kutosha wakihakikisha kuwa Mc alobobea katika fani ''Mwana wa Mshikemshike akitabasam mda wote mithili ya Mkandamizaji Ng'wanawane!!!

Kosa Uchekwe!!

Harusi Ya Bw na Bi Daudi Nkinda-Carnival Hall Dsm

Tukiwa na furaha ya angalau sare na timu ya Senegal sisi wapenda soka,jioni ya tar 02 Juni tukawa na ntongeza ya sababu ya kufurahi kwa kujumuika na watu wengine kuwapongeza ndugu zetu Bw na Bi Daudi pale ndani ya viunga vya Sabasaba..
Hiyo ilikuwa ni sherehe iliofuatia maneno ya ''....ndio nakubali...'' kutoka kwa vinywa vya wapendanao hao pale kanisa la AIC-Magomeni.
Ilikluwa ni burudani ya kutosha kwa wachaga wale kwa kumuoza binti yao kwa wasukuma.Ni furaha ilioje!
''...Kubyaaaaala cha wizaaaaaa...''
Vigelegele na nderemo za kutosha kabisa vikatawala na kuleta uhondo uku vichombwezo vya Mwana wa Mshikemshike vikitia nakshi ukumbi ule wa Carnival.

Thursday, May 31, 2007

SEND OFF PARTY YA BI FLORA-AIRPORT NIGHT PARK


Aiingia kwa tabasamu la haja bi arusi mtarajiwa! akitembea kama anagombea nafasi ya kuiwakilisha nchi katika Miss World Beuty Contest!! huku akisindikizwa na mpambe wake wakiwa wamependeza na rangi nzuri ya pitch!! ingawa walichelewa kidogo kuingia ukumbini,kufuatia shughuli za kimila kuxhelewa kufikia ukingoni jioni ile,McNdimbo kama kawaida yake akaipeleka shughuli kwa ku-keep time! wakaanza kwa kufungua champaign af wakala keki na baadae utambulisho na nasaha fupi zilizoofuatiwa na burudani za kutosha kutoka upareni.. ''....ambiere ee.....mgothi eee.....'' wakaruka na sebene za kiroho na baadae wakaenda kula na kupata burudani ya show za wateule wa Mungu na mtaalam wa kuiga sauti za watu Bw Nyerere! Ama kwel "... burudani ni jadi yetu..."

Sunday, April 8, 2007

HARUSI-MOROGORO HOTEL

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mwana wa Mshikemshike kwa mwaka 2006 kutua Mji kasoro bahari na kuibukia Morogoro Hotel kuendesha shughuli iloandaliwa na ikaandalika ya Bw na Bi Cathbert Chilongani!
''....tunapotaka sisi ni hapo tuuuu...''
wangoni wakijimwayamwaya na vionjo vya nyumbani na kupiga vigelegele na huku viti vyao vikionekana havina kazi kwani kila mda walionekana wakiruka vilivyo hapokwa ukumbi na huku Mc akiwapa uhondo wa kutosha na kuifanya sherehe kuwa kweli ka wahenga wanavyosema ''...upele umemkuta mkunaji...''

HARUSI- HILL PARK

Ndani ya viunga vya Chuo Kikuu Dar es salaam,karibu na Car Park No.2 Sauti yenye bashasha na isiyochosha kuisikia ya McNdimbo ilisikika
''..ladies and gentleman I present to you the Bride and Grooom!!!....''
Vigelegele na shangwe na vifojo vikasikika na huku sura za tabasam za Bw na Bi Japhet Minja wakiingia na kusindikizwa na tarumbeta kutoka Bombo Family..
Ilikuwa ni burudani na furaha tosha kabisa ndani ya Hill Park

SEND OFF-BEACHCOMBER

Pembezoni kabisa mwa jiji la Dar es salaam,katika ufukwe wa bahari ya Hindi,upepo mwanana ukivuma na kuruhusu wageni wapatao 200 kjisikia peponi kwani walikuwa wamezunguka bwawa la kuogelea la Hotel nzuri ya BeachComber huku kwa shauku kubwa wakimsubiri mrembo Bi Violet Rutashobya aingie na wapate fursa ya kumuaga.
Kazi nzuri ya upambaji kutoka Dotinata Decoration na burudani tosha ya muzik kutoka Vuje Disco Sound vilitosha kumfanya Mwana wa Mshikemshike aongee kwa kujiamini kuwainua wageni hao ili kumpokea Mtarajiwa huyo aliyepambwa na kupambika pale Sinza Mori Mary Saloon....
Hoihoi na nderemo hazikupotea baada ya hapo kwani burudani ndo ilikuwa jadi ya hapo!!

ARUSI - USHIRIKA MOSHI

Ilikuwa ni shangwe na vigelegele pale Bw Elieza Msuya akiwa anaingia ndani ya ukumbi wa Chuo Cha Ushirika mjini Moshi huku kamshikilia mkewe,Bi Elizabeth,kana kwamba kuna mtu atamuiba!!
Ukumbi ukiwa umepambwa na mpambaji maarufu mjini Moshi-Mama Dear,huku burudani ya mziki iktoka bila kubughudhi maskio ya waalikwa ikiletwa na Dj Athumani mwenye makao yake apo Stand ya mabasi.
Mwana wa Mshikemshike kutoka jijini Daaaar es salaam akiunguruma kwa sauti yake adimu na vipande vya vijimaneno flani ivi vya apa napale yaaani ilikuwa ni burudani tosha kabisa!

Saturday, March 25, 2006

ARUSI-SAME SECONDARY SCHOOL HALL

Bw Daniel Mnzzava na mkewe Bi Huruma waliingia na kusindikizwa na tarumbeta zahapo kanisa la KKKT dayosisi ya Same...Wapare wakisubiri kwa hamu kubwa kushuhudia kazi nzuri ya Mwana wa Mshikemshike( wanamuita Mc wa Bongo ).Bila ya ajizi nae kwa kushirikiana na Dj mdogo kabisa wakawapa uhondo wa kipare na vionjo vya kiafrika na kidhungu ati! wakawarusha vilivyo na kubaki kuwa gumzo katika anga zile za wadidu!!

Saturday, February 28, 2004

BURUDANI NA KUMBUKUMBU UNDER ONE ROOF

MUZIK, TRUMPETS, VIDEO SHOOTING AND STILL PICTURES