Tuesday, June 5, 2007

Harusi Ya Bw na Bi Daudi Nkinda-Carnival Hall Dsm

Tukiwa na furaha ya angalau sare na timu ya Senegal sisi wapenda soka,jioni ya tar 02 Juni tukawa na ntongeza ya sababu ya kufurahi kwa kujumuika na watu wengine kuwapongeza ndugu zetu Bw na Bi Daudi pale ndani ya viunga vya Sabasaba..
Hiyo ilikuwa ni sherehe iliofuatia maneno ya ''....ndio nakubali...'' kutoka kwa vinywa vya wapendanao hao pale kanisa la AIC-Magomeni.
Ilikluwa ni burudani ya kutosha kwa wachaga wale kwa kumuoza binti yao kwa wasukuma.Ni furaha ilioje!
''...Kubyaaaaala cha wizaaaaaa...''
Vigelegele na nderemo za kutosha kabisa vikatawala na kuleta uhondo uku vichombwezo vya Mwana wa Mshikemshike vikitia nakshi ukumbi ule wa Carnival.

No comments: