Tuesday, June 5, 2007

Juni 16 Ndo hiyoooooo!!


Ushawahi kuona mganga akajiganga!

Mbado!

Ushawahi kuona kinyozi anajinyoa tena ndani ya daladala!

Basi hayo ndo mambo ya Jun 16 pale ambapo McNdimbo almaarufu Mwana wa Mshikemshike atakapokua mbele ya altare pale CCT Chamlaincy-UDSM akiatamka kwa lugha ya kikwao

''...Yes I do...'' Huku kimwana wake alobarikiwa na Mwenyeeezi Mungu,mtoto mwenye mvuto na tabasamu la asili akinyoosha kidole chake cha mkono wa kushoto na kuvikwa ile golden wedding ring!

Wajua kitachofuata? ni vigelegele na makofi na vifijo na nderemo na ......

kutoka Mbeya na Arusha na Singida na Dodoma na Songea na Bukoba na Mwanza na hapahapa jijini af vya ziada kutoka kule USA

Ni burudani ya kutosha sasa itakayofuatia pale Sinza Kijiweni kwa Vatcan City Hall na hao waburudishaji wa kutosha wakihakikisha kuwa Mc alobobea katika fani ''Mwana wa Mshikemshike akitabasam mda wote mithili ya Mkandamizaji Ng'wanawane!!!

Kosa Uchekwe!!

Harusi Ya Bw na Bi Daudi Nkinda-Carnival Hall Dsm

Tukiwa na furaha ya angalau sare na timu ya Senegal sisi wapenda soka,jioni ya tar 02 Juni tukawa na ntongeza ya sababu ya kufurahi kwa kujumuika na watu wengine kuwapongeza ndugu zetu Bw na Bi Daudi pale ndani ya viunga vya Sabasaba..
Hiyo ilikuwa ni sherehe iliofuatia maneno ya ''....ndio nakubali...'' kutoka kwa vinywa vya wapendanao hao pale kanisa la AIC-Magomeni.
Ilikluwa ni burudani ya kutosha kwa wachaga wale kwa kumuoza binti yao kwa wasukuma.Ni furaha ilioje!
''...Kubyaaaaala cha wizaaaaaa...''
Vigelegele na nderemo za kutosha kabisa vikatawala na kuleta uhondo uku vichombwezo vya Mwana wa Mshikemshike vikitia nakshi ukumbi ule wa Carnival.