Sunday, November 18, 2007

HARUSI YA BW. RICHARD MASUKE NA BI DINNA-Peace Of Mind TPDC Mikocheni tar 17 Nov,2007

"..kubyaala mawe,kubyaala cha widza..."
ilikuwa ni uhondo kutoka kwa DJ TEN akiwakamata wasukuma kwa kina walipokuwa wakiwa na furaha ya kupata binti mrembo mwenye asili ya kijita,aliyezamia mitaa ya Bariadi siku tele na kuwa na ladha ya kisukuma pia-Dinna..mweupe na ambaye kwa mila za kisukuma basi hiyo mahali yake ukiwa namfuko mwepesi hugusi. Ila kijana Richard akajipindua na kumtia kibindoni kwa furaha za ziada.
"...ndolelaaaaa...ndolela babaaaa...!" wasukuma wa kijita hao wakazunguka nao wakijifariji baada ya binti yao kuungana na familia ya kina Masuke.Wakicheza kwa furaha na kuongozwa na Ephraim Mafuru(Marketing manager wa Vodacom Tanzania),paliwa hapatoshi!!
Mtaalamu wa burudani McNdimbo,kama kawaida akiwapa wakati mgumu weasukuma wala kuketi katika viti vyao kila baada ya muda! kwa kweli ilikuwa burudani kwelikweli.
Shughuli hiyo ilisheheni wadau wa kutosha akiwamo Waziri wa mifugo,Mh.Diallo

No comments: