Sunday, November 18, 2007

SEND OFF PARTY YA BI.ABELA KAJUMULO LANDMARK HOTEL TAR 8,NOV,2007

Ilikuwa ni nderemo na furaha kwa wahaya wale na kuwa na uhakika na kupata mume tena wa kinyumbani! ilikuwa ni '...dereva babili...dereva babiliii eee...!' kili baada ya muda. wazazi wakiwa na furaha kweli na hasa Mama wa bibi arusi mtarajiwa a.k.a mama Tina,ambaye pia ni mama yake na mwigizaji maarufu wa filamu hapa nchini-Kanumba(ambaye alikuapo pia).
Shughuli ilianza na taratibu za mila na desturi za kihaya,wakwe wakaingia na mizigo ya kutosha;kabiya(beer),kasoda,bila kusahau kabhitoki(ndizi) na kakinywaji ka nyumbani. Ilikuwa ni burudani sana kuona wahaya hao,pamoja na usomi wao uliobobea,wakizama katika mila na desturi zao.
Baada ya majadiliano marefu ya hapa na pale kati ya mshenga na wazazi wa binti mtarajiwa waliruhusiwa kumleta bwana mtarajiwa ndani na kisha bi mtarajiwa akaingia kwa mbwembwe na shughuli ikaenda murua chini ya mikono salama ya mtaalam wa kuburrudissha hapa Africa ya mashariki na kati-McNdimbo 'mwana wa mshikemshike'
Pamoja nae alikuwapo Dr. Zero 'mzee wa dozi nene' kwa maharusi na show yake kali yenye vionjo vyote vya burudani;bongo flava,gospel,zilipendwa hadi segere! kudadadeki!!
ilikuwa ni uhondo toshaaa!

No comments: