Sunday, April 8, 2007

HARUSI-MOROGORO HOTEL

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mwana wa Mshikemshike kwa mwaka 2006 kutua Mji kasoro bahari na kuibukia Morogoro Hotel kuendesha shughuli iloandaliwa na ikaandalika ya Bw na Bi Cathbert Chilongani!
''....tunapotaka sisi ni hapo tuuuu...''
wangoni wakijimwayamwaya na vionjo vya nyumbani na kupiga vigelegele na huku viti vyao vikionekana havina kazi kwani kila mda walionekana wakiruka vilivyo hapokwa ukumbi na huku Mc akiwapa uhondo wa kutosha na kuifanya sherehe kuwa kweli ka wahenga wanavyosema ''...upele umemkuta mkunaji...''

HARUSI- HILL PARK

Ndani ya viunga vya Chuo Kikuu Dar es salaam,karibu na Car Park No.2 Sauti yenye bashasha na isiyochosha kuisikia ya McNdimbo ilisikika
''..ladies and gentleman I present to you the Bride and Grooom!!!....''
Vigelegele na shangwe na vifojo vikasikika na huku sura za tabasam za Bw na Bi Japhet Minja wakiingia na kusindikizwa na tarumbeta kutoka Bombo Family..
Ilikuwa ni burudani na furaha tosha kabisa ndani ya Hill Park

SEND OFF-BEACHCOMBER

Pembezoni kabisa mwa jiji la Dar es salaam,katika ufukwe wa bahari ya Hindi,upepo mwanana ukivuma na kuruhusu wageni wapatao 200 kjisikia peponi kwani walikuwa wamezunguka bwawa la kuogelea la Hotel nzuri ya BeachComber huku kwa shauku kubwa wakimsubiri mrembo Bi Violet Rutashobya aingie na wapate fursa ya kumuaga.
Kazi nzuri ya upambaji kutoka Dotinata Decoration na burudani tosha ya muzik kutoka Vuje Disco Sound vilitosha kumfanya Mwana wa Mshikemshike aongee kwa kujiamini kuwainua wageni hao ili kumpokea Mtarajiwa huyo aliyepambwa na kupambika pale Sinza Mori Mary Saloon....
Hoihoi na nderemo hazikupotea baada ya hapo kwani burudani ndo ilikuwa jadi ya hapo!!

ARUSI - USHIRIKA MOSHI

Ilikuwa ni shangwe na vigelegele pale Bw Elieza Msuya akiwa anaingia ndani ya ukumbi wa Chuo Cha Ushirika mjini Moshi huku kamshikilia mkewe,Bi Elizabeth,kana kwamba kuna mtu atamuiba!!
Ukumbi ukiwa umepambwa na mpambaji maarufu mjini Moshi-Mama Dear,huku burudani ya mziki iktoka bila kubughudhi maskio ya waalikwa ikiletwa na Dj Athumani mwenye makao yake apo Stand ya mabasi.
Mwana wa Mshikemshike kutoka jijini Daaaar es salaam akiunguruma kwa sauti yake adimu na vipande vya vijimaneno flani ivi vya apa napale yaaani ilikuwa ni burudani tosha kabisa!